Matokeo ya uchaguzi huo unaofanyika kwa awamu mbili, na utakaomalizika Julai 7, huenda yakatikiza masoko ya Ulaya, uungaji mkono wa magharibi wa Ukraine, pamoja na uwezo wa nyuklia na kijeshi wa Ufaransa.
Wafaransa wengi wameghadhabishwa na mfumuko wa bei, kudorora kwa uchumi, pamoja na utawala wa Rais Emmanuel Macron, ambao wanaouna kama usiozingatia maslahi ya mwananchi wa kawaida. Chama cha upinzani kinachopinga uhamiaji cha National Rally kimefanya kampeni kubwa kupitia majukwaa ya kimitandao kama vile tiktok, huku kikionekana kuongoza kwenye ukusanyaji wa maoni.
Muungano mpya wa mrengo wa kushoto wa New Popular Front, pia ni changamoto kubwa kwa muungano wa Macron wa Together for the Republic, unaounga mkono wafanyabiashara.
Kuna jumla ya wapiga kura milioni 49.5 watakaochagua wabunge 577 kwenye baraza la chini, la bunge la kitaifa lenye ushawishi, kupitia duru mbili za uchaguzi.