Hili linajiri siku moja baada ya kukamatwa kwake ambako kulichochea maandamano yaliyogubikwa na ghasia kote nchini.
Baadhi ya vyombo vya habari vimenukuu vyanzo ambavyo hawakuvitaja, lakini vilisema waendesha mashtaka walitaka Khan arudishwe rumande kwa siku 14.
Wanasiasa wa Pakistan wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara na kuwekwa rumande tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1947, lakini ni wachache walilipinga moja kwa moja jeshi ambalo limefanya angalau mapinduzi matatu na kutawala kwa zaidi ya miongo mitatu.
Baadhi ya waandamanaji walionyesha hasira zao kwa wanajeshi wakichoma moto makazi ya makamanda wa jeshi mjini Lahore na kuzingira lango kuu la makao makuu ya jeshi katika mji wa Rawalpindi.
Polisi imeamua kupambana na wafuasi wa chama cha Khan cha PTI katika miji kote nchini kwa saa kadhaa Jumanne usiku.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti vifo viwili katika mapambano mawili , wakati polisi inasema watu 945 waliovunja sheria wamekamatwa katika jimbo la Punjab pekee ambalo ni maarufu nchini humo.