Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 11:06

Pakistan imeweka marufuku ya utangazaji wa hotuba na mikutano ya Imran Khan


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan

Vizuizi hivyo vilivyotolewa Jumapili jioni vililaaniwa na wakosoaji kuwa ni shambulio dhidi ya uhuru wa kuzungumza  nchini humo pamoja na vyombo huru vya habari wakiitaka serikali iondoe hatua hiyo

Pakistan imeweka marufuku kamili ya utangazaji wa hotuba na mikutano ya waandishi wa habari inayofanywa na Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan na haraka kukisimamisha kituo kikuu cha televisheni cha satelaiti kwa kukaidi agizo hilo.

Vizuizi hivyo vilivyotolewa Jumapili jioni vililaaniwa na wakosoaji kuwa ni shambulio dhidi ya uhuru wa kuzungumza nchini humo pamoja na vyombo huru vya habari wakiitaka serikali iondoe hatua hiyo.

Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Habari vya Kielektroniki ya Pakistan iliamuru vituo vyote vya televisheni vya satelaiti kuacha kuonyesha hotuba za Khan za "moja kwa moja na zilizorekodiwa" pamoja na mazungumzo ya vyombo vya habari mara moja ikionya kuwa wanaokiuka agizo hilo watafutiwa leseni zao.

Marufuku hiyo imekuja saa chache baada ya Khan, mwenye umri wa miaka 70, kuwahutubia wafuasi wa chama chake cha upinzani cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), nje ya makazi yake katika mji wa mashariki wa Lahore na alishutumu ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu Shehbaz Sharif.

XS
SM
MD
LG