Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 04:16

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan ajeruhiwa katika jaribio la mauaji


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan akisaidiwa baada ya kupigwa risasi mguunin huko Wazirabad, Pakistani Novemba 3, 2022. (REUTERS)
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan akisaidiwa baada ya kupigwa risasi mguunin huko Wazirabad, Pakistani Novemba 3, 2022. (REUTERS)

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan alijeruhiwa katika jaribio la mauaji Alhamisi alipokuwa akiongoza maandamano yake yanayoendelea dhidi ya serikali huko Islamabad.

Kiongozi huyo maarufu wa chama cha upinzani Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) mwenye umri wa miaka 70 alipigwa risasi moja kwenye mguu wake wa kulia, msaidizi wake mkuu Rauf Hassan alithibitishia VOA. Shambulio hilo la bunduki katika mji wa Wazirabad, jimbo la kati la Punjab, lilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 14 kujeruhiwa, akiwemo waziri mkuu huyo wa zamani.

Khan alisafirishwa hadi hospitali ya Lahore, mji mkuu wa Punjab, takriban kilomita 150 kutoka eneo la shambulizi, ambapo madaktari walisema yuko katika hali nzuri, kulingana na msaidizi.

Picha za video zilionyesha mtu mwenye bunduki akimfyatulia risasi kutoka chini Khan ambaye alikuwa juu ya lori lililotengenezwa kwa makusudi ya mkutano akiongoza maandamano hayo. Walioshuhudia walisema mwandamanaji mmoja alijaribu haraka kumzuia mtu huyo anayeshukiwa kuwa mpiga risasi huku akiwa bado anafyatua risasi kwa kutumia silaha yake ya rashasha na kumuuwa mtu mmoja aliyekuwa akiandamana.

Polisi baadaye walimkamata mshukiwa huyo na kumweka chini ya ulinzi. Katika video iliyodaiwa kuwa ya kukiri makosa iliyotolewa baadaye kwa waandishi wa habari, mshukiwa alisema alitenda kosa hilo peke yake na kwamba dhamira yake pekee ilikuwa kumuua Khan kwa kupotosha umma.

XS
SM
MD
LG