Vita vya Sudan: Wakaazi wa Wad Madani huenda wakaukimbia mji huo uliokumbwa na mapigano

Watu wakiwa kwenye foleni nje ya Ofisi za Pasipoti na Huduma za Uhamiaji ndani huko Wad Madani Septemba 3, 2023. picha na AFP

Jeshi la Sudan limekuwa likipambana na vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) siku ya Ijumaa karibu na mji wa Wad Madani, ambao umekuwa ukitumiwa na raia kama hifadhi wakati wa mapigano, maelfu ya raia waliingia mjini humo katika kipindi cha miezi nane ya vita.

Mapigano katika eneo hilo lililoko kiasi cha kilometa 170 kusini mashariki mwa Khartoum, na kutishai kuanzisha mapigano mapya katika mzozo uliowakosesha makazi takriban watu milioni saba, na kuuacha mji mkuu ukiwa umeharibiwa na hivyo kuchochea wimbi la mauaji ya kikabila huko Darfur.

Kuchukuliwa kwa mji wenye idadi kubwa ya watu wa Wad Madani, ambako kuna baadhi ya ofisi za huduma za serikali na misaada, zimesababisha uwezekano mkubwa kwa watu wengi kupoteza makazi yao na mgogoro wa kibinadamu kuwa mkubwa zaidi ambapo Umoja wa Mataifa umeonya kuwepo kwa hali inayofanana na janga la njaa katika maeneo yaliyoathiriwa na vita.

Kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya picha ambazo zimesambazwa zikiwaonyesha watu wakipanga vitu vyao wakati wengine wakiulizia njia salama za kutoka nje ya mji huo wa Wad Madani.

Wakazi mjini Khartoum na miji mingine wameripoti ubakaji, uporaji, mauaji ya kienyeji na kuwekwa vizuizini kunakofanywa na vikosi vya RSF.

Kundi la wanamgambo wa RSF, ambalo katika siku za hivi karibuni limepata kasi, ikiwa pamoja na kukamata miji mikuu, limesema linajaribu kuwalinda raia.

Katika taarifa yake kundi hilo limesema kuwa linataka kuvunja ngome za jeshi na wakazi wa Wad Madani na maeneo yanayozunguuka jimbo la El Gezira wanataka wapewe uhakikisho.

Walioshuhudia katika mji wa Wad Madani wamesema waliweza kusikia milipuko, lakini hakuna mapigano ndani ya mji

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters