Baada ya miezi kadhaa ya wasiwasi na kushindikana kwa mazungumzo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken aliwasilisha matokeo kufuatia tathmini ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani.
Waziri Blinken, amesema jeshi la Sudan na vikosi vya akiba vya RSF, ambavyo mvutano wao wa muda mrefu ulikuwa na kusababisha ghasia kubwa Aprili 15, vimefanya uhalifu wa kivita.
RSF pia imefanya mauaji ya kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu, amesema, akizungumzia mauaji ya kimbari yaliyofanywa na kikosi kikubwa cha Waarabu na wanamgambo washirika wake dhidi ya watu wa kabila la kiafrika la Masalit huko Darfur.
Forum