Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:11

Msafara wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu washambuliwa Khartoum


Familia za Wasudan zikipanda roli kwenda Misri baada mapigano kuzuka katika mji mkuu wa Khartoum. Picha na REUTERS/Heba Fouad
Familia za Wasudan zikipanda roli kwenda Misri baada mapigano kuzuka katika mji mkuu wa Khartoum. Picha na REUTERS/Heba Fouad

Watu wawili wameuwa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulizi kwa msafara wa kibinadamu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ICRC imesema Jumapili.

Waliojeruhiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu wa ICRC, Shirika la Msalaba Mwekundu limesema katika taarifa yake.

“Msafara wa kibinadamu, unajumuisha magari matatu ya ICRC na mabasi matatu, yote yakiwa na alama zilizokuwa zikionekana za nembo ya Msalaba Mwekundu, ambayo yalitarajiwa kuwahamisha mamia ya raia walio katika mazingira hatarishi kutoka Khartoum kwenda Wad Madani, wakati msafara huo uliposhambuliwa ulikuwa ukiingia katika eneo la kuwahamisha watu, taarifa ilisema.

Haijaulaumu upande wowote, lakini jeshi la Sudan limesema msafara huo ulishambuliwa baada ya kukiuka makubaliano kwa kuelekea maeneo yao ya ulinzi, wakitumia gari “lililokuwa linamilikiwa na waasi” — ikiimanisha kikosi cha dharura (RSF)

Katika taarifa tofauti, Kikosi cha RSF kimelishutumu jeshi kwa kuushambulia msafara huo .

Kiongozi wa Kikosi cha Dharura Mohamed Hamdan Dagalo akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari.huko Khartoum. Picha na REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Kiongozi wa Kikosi cha Dharura Mohamed Hamdan Dagalo akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari.huko Khartoum. Picha na REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Wakati huo huo Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Jeshi la Sudan na kikosi hasimu cha wanamgambo waliokuwa katika mapigano kwa miezi nane, hawakubaliani na tangazo lilitolewa na wapatanishi wa kikanda kuwa wamebubali kusitisha mapigano na kufanya mazungumzo ya kisiasa.

IGAD, kundi la mataifa ya Afrika Mashariki, Marekani pamoja na Saudi Arabia wamekuwa wakitaka kuwapatanisha ili kuumaliza mgogoro huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 12,000, na kusababisha watu zaidi ya milioni 6.5 kupoteza makazi, na kuifanya nchi hiyo ikumbwe na hali mbaya ya uchumi.

IGAD imesema siku ya Jumapili kuwa mkuu wa jeshi la Sudan jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa kikosi cha dharura Mohamed Hamdan Dagalo wamekubali kukutana kwa mara ya kwanza tangu mapigano yazuke pamoja na kukubali pendekezo la kusitisha mapigano bila masharti.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa Port Sudan August 27, 2023. Picha na REUTERS/Ibrahim Mohammed Ishak
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa Port Sudan August 27, 2023. Picha na REUTERS/Ibrahim Mohammed Ishak

Lakini katika taarifa hiyo ya Jumapili, jeshi linalofanyakazi na Wizara ya Mambo ya Nje lilisema kuwa haliitambui taarifa iliyotolewa na IGAD wakati haikujumuisha maelezo iliyoyatoa. Ikizingatiwa kuwa mkutano huo na Dagalo ulikuwa na sharti la sitisho la kudumu la mapigano na kuondoka kwa vikosi vya RSF katika mji mkuu wa Khartoum.

Wakati huo huo, vikosi vya RSF vimesema kuukubali mkutano huo kulikuwa na sharti kuwa Burhan hatahudhuria kwa wadhifa wake wa ukuu wa nchi, nafasi ambayo amekuwa akiishikilia tangu mwaka 2019, wakati jeshi na RSF walipokuwa wakifanyakazi pamoja kumuondoa kiongozi jasiri wa muda mrefu Omar al-Bashir.

Jeshi ambalo linaona vita kama ni uasi uliofanywa na RSF, ni vigumu kukubaliana na matakwa ya aina hiyo.

Mazungumzo yaliyoongozwa na Saudi Arabia na Marekani yalisimaisihwa mapema mwezi huu bila kuwepo maendeleo kwa makubaliano ya awali ya kujenga matumanini au kusitisha mapigano.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG