Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:39

Baraza la usalama la UN linapiga kura kumaliza operesheni za kisiasa Sudan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika moja ya vikao vyake hivi karibuni mjini New York. November 10, 2023.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika moja ya vikao vyake hivi karibuni mjini New York. November 10, 2023.

Vita vilizuka Aprili 15 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces, baada ya wiki kadhaa za mivutano mkali kati ya pande hizo mbili juu ya mpango wa kuunganisha vikosi kama sehemu ya utawala wa mpito kutoka utawala wa kijeshi hadi demokrasia ya kiraia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura Ijumaa kumaliza operesheni za kisiasa nchini Sudan iliyokumbwa na vita, wanadiplomasia wamesema, baada ya kaimu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, alipo-omba hatua hiyo mwanzoni mwa mwezi huu na alielezea utendaji kazi wa ujumbe “unasikitisha”.

Vita vilizuka Aprili 15 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces, baada ya wiki kadhaa za mivutano mkali kati ya pande hizo mbili juu ya mpango wa kuunganisha vikosi kama sehemu ya utawala wa mpito kutoka utawala wa kijeshi hadi demokrasia ya kiraia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alielezea hali hiyo kwa waandishi wa habari siku ya Jumanne, kwamba “Una majenerali wawili ambao wanapuuza kabisa maslahi ya watu wao”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Alipoulizwa iwapo mgogoro huo ni kushindwa kwa Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika, Guterres alisema “Ni wakati wa kutafuta suluhisho. Hili ni kosa la wale ambao walijitolea kwa maslahi ya watu wao kwa ajili ya mapambano ya madaraka.

Rasimu ya azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, inasitisha jukumu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa, unaojulikana kama UNITAMS, hapo Disemba 3 na inahitaji kusitishwa kwa miezi mitatu ijayo. UNITAMS ilianzishwa na baraza la wanachama 15 mwezi Juni 2020 ili kutoa msaada kwa Sudan wakati wa kipindi chake cha mpito wa kisiasa kuelekea utawala wa kidemokrasia.

Timu ya Umoja wa Mataifa inayotoa misaada ya kibinadamu na maendeleo itaendelea kuwepo nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG