Michezo ya Olimpiki mwaka huu nchini Paris ilifunguliwa wakati ikizua utata mkubwa miongoni mwa makundi ya kidini ikiwemo Vatican. Mengi ya makundi hayo yalilalamikia kile walichosema kuwa kenjeli ya chakula cha mwisho cha Yesu na watumishi wake, ingawa waandaji wamepinga madai hayo wakisema kuwa ufunguzi huo uliendana na picha iliochorwa na Leonardo da Vinci.
Kando na utata huo, kuna hema lililotengenezwa karibu na kijiji cha wanariadha mjini Paris, ambapo viongozi wa kidini kutoka dini 5 kubwa ulimwenguni wanatoa huduma za kiroho kwa wanariadha wanaoshirikia michezo hiyo.
Wawakilishi wa dini za Budhaa, Hindi, Kikiristo, Kiislamu na Kiyuda walitumia miezi kadhaa kuunda eneo hilo, ambapo zaidi ya wanariadha 10,500 pamoja na wasaidi wao wanaweza kupata msaada wa Imani, pamoja na kuabudu.