Viongozi wa Afrika wahudhuria Ibada ya kumuaga hayati Kaunda

Hayati Kenneth Kaunda

Viongozi wa Kiafrika Ijumaa wameungana na raia wa Zambia, kwa ibada ya maombolezi, ya Kenneth Kaunda.

Kaunda ni rais mwanzilishi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika, na anafahamika kwa juhudi zake za kuunga mkono uzalendo wa kiafrika.

Marais wa Kenya, Afrika Kusini, na Zimbabwe, wako mjini Lusaka, kwa heshima ya kutoa heshima zao za mwisho kwa hayati Kaunda, ambaye alifariki mwezi Juni, akiwa na umri wa miaka 97.

Kaunda anakumbukwa kwa kuongoza Zambia kupata uhuru wake, kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza, mnamo mwaka 1964.

Pia anafahamika kwa mchango wake wa kuunga mkono harakati za ukombozi, ambazo zilipelekea kupatikana kwa uhuru wa nchi kama Angola, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe.

Jeshi la Zambia limepeleka mwili wake, katika majimbo 10 ya nchi hiyo, ili raia kutoka maeneo yote ya nchi, waweze kutoa heshima zao za mwisho.

Chanzo cha Habari : VOA News/ AFP