Uvamizi wa Congress wawakumbusha wahamiaji Marekani machungu waliowahi kupitia

Maafisa wa polisi wa Bunge la Marekani wakiwazuia waandamanaji wanaojaribu kuvunja mlango wa Bunge Jumatano, Jan. 6, 2021, in Washington. (AP Photo/Jose Luis Magana)

Vitendo viovu vya kulivamia Bunge la Marekani limetoa somo makini kwa Gigi Mei, aliyehitimu masomo mwezi Mei mwaka 2020 kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, New York.

“Demokrasia iko katika mashaka ya kweli, na inachukuwa nguvu nyingi na juhudi kubwa,” amesema Mei, mwenye miaka 25 kutoka China. “Na inahitaji watu katika kila nyanja kuiendeleza, kuilinda na kuitekeleza.”

Mei ni kati ya darzeni ya wahamiaji wa Marekani au kizazi cha kwanza cha Wamarekani alizungumza na Sauti ya Amerika baada ya maelfu ya wafanya ghasia walipo washinda nguvu na kuwapita maafisa wa polisi wa Bunge la Marekani katika hatua iliyokuwa haijafanikiwa kuwazuia wabunge kurasmisha ushindi wa Joe Biden dhidi ya Donald Trump kama rais anayefuatia.

Gigi Mei

Kama ilivyo sehemu nyingi ulimwenguni, wahamiaji hawa walieleza kushtushwa na uvamizi wa kutumia silaha wa Januari 6, uliowaacha watu watano kufariki, akiwemo afisa wa polisi.

Baadhi walifananisha na ghasia za kisiasa katika nchi ambazo wametoka. Walizungumzia mpasuko wa kisiasa – uliochafuliwa zaidi na uchaguzi wa Novemba 3, kesi za wizi wa kura zilitupiliwa mbali katika mahakama za jimbo na mahakama za serikali kuu, kukiwa hoja mpya ya kufungua kesi ya kumshtaki rais kumuondoa madarakani na vitisho vya machafuko nchi nzima wakati wa tarehe ya kuapishwa Biden Jumatano.

Hata hivyo wahamiaji hao pia wamesema walikuwa wanaamini kuwa demokrasia itashinda nchini Marekani – lakini kwa jitihada.

“Tunaona Marekani inatumia mabilioni ya dola… katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali” kuunga mkono demokrasia, maendeleo ya uchumi, elimu ya kiraia, haki za binadamu na zaidi ya h apo, amesema Mirwais Safi, aliyekuwa mkalimani wa serikali ya Marekani katika nchi yake alikotoka Afghanistan kabla ya kuja Marekani kwa kutumia visa maalum ya wahamiaji. “Lakini tumekuta bado kazi kubwa inahitajika kufanyika nchini Marekani.

Hivi sasa Safi anafanya kazi katika kampuni isiyokuwa ya kibiashara kaskazini mwa Virginia – ikiangazia demokrasia na maendeleo.

FILE - In this Jan. 6, 2021, Wafuasi wa Rais Donald Trump wakikabiliwa na maafisa wa polisi wa Bunge la Marekani nje ya ukumbi wa Baraza la Seneti ndani Congress Washington.

UKWELI USIOPENDEZA

Naye Boukary Sawadogo, anayefundisha masomo ya filamu za Afrika katika Chuo cha City College, New York, picha ya ghasia za uvamizi wa Congress “zilionekana kama ni filamu ya Hollywood” – na sio hakika ambayo angetegemea jambo hilo kutokea katika jengo la kitovu cha siasa za Marekani.

Sawadogo, aliyekulia Burkina Faso, amesema ilimkumbusha maandamano ya umma ya 2014 yaliyomshinikiza rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuachia madaraka, Blaise Compaore, baada ya miaka 27. Waandamanaji waliliteka bunge, wakachoma moto jengo,” alisema. Wabunge walikimbia “kuokoa maisha yao.”

Wabunge wa Marekani pia walikimbizwa kutoka katika ukumbi wa mikutano lakini walirejea tena baada ya saa kadhaa kuendelea na kurasmisha matokeo ya uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa.

Watu waliokuwa katika kundi lililovamia Bunge walisema walikuwa na haki ya kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa Marekani.

“Tuko kudai ukweli,” amesema Tuan Anh La, Mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Majini la Marekani mwenye asili ya Vietnam. “Haiwezekani sisi kukubali baadhi ya matokeo wakati nusu ya wapiga kura wako mashakani” kutokana na kura ya Novemba 3.

Masanduku yenye kura za wajumbe yakiingizwa katika Baraza la Wawakilishi.

Electoral College ballot boxes are carried to the House of Representatives at the U.S. Capitol in Washington, D.C., Jan. 6, 2021.

Individual states took days, even weeks, to count ballots. In the end, Biden received 81 million votes; Trump got 74 million. In the determinative U.S. Electoral College, Biden defeated Trump 306-232 votes.

Kila jimbo lilichukuwa siku kadhaa, hata wiki kadhaa, kuhesabu kura. Hatimaye, Biden alipata kura milioni 81 ; Trump akapata kura 74 milioni. Katika Kura za Wajumbe zinazoamua mshindi maarufu kama Electoral College, Biden alimshinda Trump kwa kura 306 -232.

Vanndhath Man, aliyehamia Marekani kutoka Cambodia na anafanya kazi ya uuguzi Kaskazini mwa Virginia, amesema haamini uvamizi wa Congress ulikuwa umepangwa – japokuwa baadhi ya waandamanaji walikuja na vilipuzi, pingu na vifaa mbalimbali ikionyesha kulikuwa na mpango kabambe wenye nia mbaya.

“Nafikiri genge hili au waandamanaji hawa … hawakuwa wamepanga tukio hili kuwa la uvunjifu wa amani,” amesema. “Lakini pale palipo patikana shinikizo, ilifikia hali ya kugeuka kuwa ni uvamizi wa Bunge la Marekani.

The Capitol attack “was very personal to me,” said Osman Ahmed, 33, who had worked there for two U.S. senators from Minnesota. “As a staffer, you couldn’t get onto the Senate floor without screening,” he said. “… I know how secure and well-kept that building is.”

Uvamizi wa Bunge ulikuwa ni jambo binafsi kwangu,” amesema Osman Ahmed, miaka 33, ambaye aliwahi kufanya kazi na maseneta wawili wa Marekani kutoka Minnesota. “Kama mfanyakazi, hukuweza kufika katika ukumbi wa Baraza la Seneti bila ya kukaguliwa,” amesema, “…najua namna jengo hilo lilivyo salama na ulinzi wake imara.”

Ahmed left in 2019, joining a Minneapolis nonprofit to build community partnerships. He recoiled from onscreen images of the Capitol’s bloodshed, which he said brought flashbacks of his childhood in an unstable Somalia.

Ahmed aliacha kazi mwaka 2019, akajiunga na shirika lisilo la kibiashara huko Minneapolis kuanzisha ushirikiano wa kijamii. Alihuzunishwa na picha za kwenye televisheni za umwagaji damu hapo Bungeni, ambazo zilimkumbusha matukio ya utotoni aliyoyaona katika nchi isiyo na utulivu ya Somalia.

Ahmed aliwapongeza “maafisa wa polisi na maafisa wa sheria waliowalinda wabunge maisha yao.” Lakini pia alisema alikuwa amesikitishwa na kitendo cha wachache kati ya waandamanaji wazungu kukamatwa --- angalau pale mwanzoni.

“Hilo linaonyesha wazi, kuwa, ubaguzi wa rangi na kukosekana usawa wa kijamii. … Na watu wa rangi --- isingekuwa hivyo ilivyotokea kama wao ndio wangekuwa wamefanya hilo.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa CNN wa takwimu za polisi Washington, watu 61 walikamatwa katika ghasia za Januari 6, ukilingansha na 316 waliokamatwa Juni 1, 2020 --- siku waandamanaji wa Black Lives Matter walipoondolewa mitaani karibu na White House kabla ya Rais Donald Trump kujitokeza kupiga picha mbele ya Kanisa la Episcopal la Mtakatifu John akishikilia bibilia.

Picha za waandamanaji wanaotafutwa na FBI zilizotolewa Jan. 8, 2021, ambao walikuwa katika Congress Jan. 6, Washington, DC.

Zaidi ya watu 70 wamefunguliwa mashtaka ya shambulizi la Bunge la Marekani na waendesha mashtaka wanafuatilia mashtaka mengine dhidi ya watu wasiopungua 100, Michael Sherwin, kaimu mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Columbia, amesema katika mkutano wa waandishi wa habari Januari 12. Amesema waendesha mashtaka waandamizi pia wanaangalia uwezekano wa kufungua mashataka ya uhaini na kusaidia hilo, ambayo yanaweza kuwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 20.

Hiyo bado ni adhabu hafifu ukilinganisha na matukio mengine kwake Jake Kim, aliyekimbia kutoka Korea Kaskazini na sasa ni mwanafunzi huko Provo, Utah.

“Kuandamana ni haki ya kidemokrasia kabisa, lakini uvunjifu wa amani unashtusha na haukubaliki,’ amesema Kim, ambaye ana umri wa miaka 30. Nchini Marekani, “ watu wanaweza kukamatwa na kutumikia kifungo kwa muda. Nchini Korea Kaskazini, watauawa.”

UHURU

Wademokrat wote na Warepublikan 10 katika Baraza la Wawakilishi la Marekani walipiga kura wiki hii kumfungulia mashtaka Trump kwa mara ya pili kitu ambacho hakijawahi kutokea, wakimshutumu kwa kuchochea vurugu.

Pia amefungiwa akaunti zake za Twitter, Facebook na mitandao mengine ya kijamii inayo mshutumu kwa matamshi yake ya uchochezi.

“Hilo linastaajabisha! Tuna uhuru wa kujieleza,” amelalamika Junior Bompeti, mwenye umri wa miaka 35 mtaalamu wa programu za kompyuta huko Dallas, Texas.

Bompeti, aliyehamia Marekani mwaka 2015 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, aliunda jamii ya Facebook ya watu wa Congo wanao muunga mkono Trump.

Alikubaliana na kesi mbalimbali ambazo hazikufanikiwa zilizotaka matokeo ya uchaguzi yabadilishwe katika majimbo mbalimbali ambapo Trump alishindwa.

“Ni lazima tuamini mchakato huo,” Bompeti amesema. “Kuna madai mengi ya wizi. Rais anaendelea kusema kulikuwa na wizi wa kura.”

UFUMBUZI

Kujenga uaminifu na demokrasia bora kunahitaji heshima, elimu na ushirikiano wa kiraia, Bompeti na wahamiaji wengine wanaeleza.

Vyama vya kisiasa lazima “waweke kando” baadhi ya tofauti zao, amesema Roba Bulga, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Brandeis aliyesomea masuala ya utatuzi wa migogoro akitokea Ethiopia. Alitaja kuwa “huu ni wakati wa maridhiano, wakati wa kuwaleta watu pamoja kama nchi.”

Roba Bulga

Anahimiza kuangalia nje ya mipaka ya Marekani, akisema, “Tishio kwa demokrasia hapa linaweza kuwa ni tishio la demokrasia katika nchi nyingine za ulimwenguni.

Mwandamanaji akichoma Bendera ya Marekanion Jumatano, Nov. 4, 2020, huko Portland, Ore. (AP Photo/Marcio Jose Sanchez)

Thavin Keo anahimiza kuwepo ustaarabu zaidi, wasiwasi juu ya “chuki zaidi kila mahala. … Angalia huko Portland. Angalia Seattle,” amesema, akigusia miezi ya maandamano ya Black Lives Matter mwaka jana ambayo baadhi ya wakati yalikuwa na mapambano ya umwagaji damu. Mkandarasi huyu mstaafu mwenye umri wa miaka 67 alikuja Marekani kama mkimbizi kutoka Cambodia mwaka 1981, na kuweka makazi yake kaskazini ya Virginia.

Thavin Keo, mzaliwa wa Cambodia aliyefanikiwa kuingia Marekani kama mkimbizi, anasema viongozi wa Republikan na Demokratik “lazima washirikiane kuendeleza demokrasia.’

Thavin Keo

” Warepublikan na Wademokrat “lazima wafanye kazi kwa pamoja kuendeleza demokrasia katika nchi hii,’

Kushirikiana katika kujenga jamii ni muhimu kwa mzaliwa wa Marekani Pahniti (Tom) Tosuksri, aliyeishi baadhi ya umri wake na wazazi wake wazaliwa wa Thailand na anafanya kazi katika programu ya kuwawezesha watu kupata nyumba za bei nafuu isiyo ya kibiashara huko Cleveland, Ohio.

Alijitolea kama muangalizi wa uchaguzi mwezi Novemba katika uchaguzi na anataka “kujihusisha zaidi … kujifunza zaidi kuhusu chaguzi za hapa nchini kwetu,” amesema.

Pia anakusudia “kuwapa moyo watu” kufanya hivyo na kujifunza zaidi kuhusu wagombea wa maeneo yao na masuala mbalimbali.

Unapopiga kura, “siyo tu kumchagua rais, siyo tu Baraza la Seneti, lakini kila kitu baina ya hayo mawili ambayo lazima tuyafahamu.”

Wahamiaji, hususan wale waliopata uraia, wana majukumu, amesema Meron Semedar, ambaye ana umri wa miaka 34 kutoka Eritrea na sasa ni mshauri wa wanazuoni wa Afrika katika Chuo Kikuu cha California- Berkeley.

“Naishawishi kila jamii ya wahamiaji kujitokeza kutekeleza haki zao,” kuanzia kukamilisha takwimu za sensa hadi kupiga kura iwapo wanastahili kufanya hivyo, Semedar amesema.

“Ni jukumu, ni wajibu, na lazima tuheshimu hilo, na kulienzi hilo. Lakini pia lazima tushiriki kuendeleza demokrasia,” amesema. “Na tuwafundishe mambo kama hayo watoto wetu. … lazima tukabidhi fikra hizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

USA, Delaware, Wilmington, Marekani , Rais mteule Joe Biden na waandishi juu ya juhudi za kupambana na virusi vya corona

Kwa upande wake Sonam Zoksang, mmiliki wa biashara ndogo huko New York kitongoji cha Hudson Valley, anasıma “demokrasia imeonyesha nguvu yake lakini inahitaji kulindwa.”

Akiwa mzaliwa wa Tibet, alikuja Marekani mwaka 1995 kupitia Nepal, ambako wazazi wake walikimbilia baada ya China kutawala nchi yao kwa mabavu.

Amesema anamuangalia Biden, rais anayeingia madarakani, atatekeleza ujumbe wake wa kuleta umoja na maridhiano.

“Naamini uongozi huu mpya na baadhi ya Warepulikan wema wanaweza kufanya kazi pamoja. Dunia inaiangalia Marekani kama ni mfano wa kuigwa.

Waandishi ni : Mariama Diallo, Carol Guensburg, Elizabeth Hughes

Ripoti hii imechangiwa na idhaa kadhaa za Sauti ya Amerika : Afghan, Cambodian, English to Africa, French to Africa, Horn, Korean, Mandarin, Somali, Thai, Tibetan and Vietnamese.