Upelelezi wa Kihistoria : Ushahidi dhidi ya Trump waanza kusikilizwa Jumatano

Rais Donald Trump

Kamati ya upelelezi katika baraza la wawakilishi Jumatano inaanza kusikiliza ushahidi wa wazi mbele ya umma juu ya kutaka kumfungulia mashtaka Rais Donald Trump wakichunguza madai kuwa alikaribisha taifa la nje kuingilia kati uchaguzi wa rais wa mwaka 2020. 

Kamati hiyo inasimamia uchunguzi huo baada ya wiki kadhaa za mikutano ya faragha ikihusisha wanadiplomasia wa zamani na wa sasa na maafisa wengine, wabunge na wale wanaoangalia nchini kote.

Mahojiano hayo yatatangazwa kupitia televisheni ambapo William Taylor mwanadiplomasia wa sasa wa juu wa Marekani nchini Ukraine na George Kent, anayesimamia masuala ya Ukraine watatoa ushahidi.

Adam Schiff alisema Taylor, Kent na shahidi mwingine wa tatu wanajiandaa kutoa ushahidi wao Ijumaa.

Marie Yovanovitch, balozi wa zamani wa Marekani huko Kyiv, ana uzoefu wa miongo kadhaa ya kazi ya heshima kwa taifa letu na ninaamini ni muhimu sana kwa Wamarekani na wabunge wote kusikia kwa maneno yao kile walichojionea na kushuhudia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.