Mageuzi yataliruhusu Bunge la Taifa kumchagua rais moja kwa moja na kuchochea khofu ya wapinzani juu ya majaribio ya kumuweka madarakani kwa muda mrefu zaidi Rais Faure Ghnassingbe.
Ofisi ya Rais waTogo Jumatano ilitangaza mashauriano zaidi kuhitajika na kusimaisha uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa uliokuwa ufanyike Aprili 20 bila ya kutoa tarehe mpya.
Baada ya wiki ya mivutano ya kisiasa juu ya marekebisho ya katiba, Gnassingbe tayari amepeleka tena sheria bungeni ili kusomwa kwa mara ya pili.
Wananchi wa Togo wamekasirika na wanataka mswaada wa kikatiba uondolewe moja kwa moja. Vinginevyo watasababisha vurugu,” amesema Nathaniel Olympio, mkuu wa chama cha upinzani cha Party of the Togolese.
“Wakati huu, mapinduzi ya kikatiba hayapita. Wakati huu watu wa Togo watasimama na kusema ‘hapana.’
Mzozo huo umechochea mjadala juu ya utawala wa Gnassingbe, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005 baada ya kumrithi baba yake ambaye mwenyewe alitawala kwa miongoni mitatu baada ya mapinduzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Uchaguzi wa bunge umewahi kucheleweshwa hapo kabla, huku upinzani ukidai kuwa bunge limetawaliwa na chama tawala wa cha Gnassingbe cha UNIR ambacho kimepotea mamlaka yake kwasababu ya ukosefu wa kura.