Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 22:06
VOA Direct Packages

Wanahabari wawili wa Togo wapewa vifungo vya jela wakati wakiwa mafichoni


Mwanahabari wa Togo akiwa mbele ya maafisa wa usalama kwenye picha maktaba.
Mwanahabari wa Togo akiwa mbele ya maafisa wa usalama kwenye picha maktaba.

Wanahabari wawili wa Togo waliopo mafichoni wamepewa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kuitusi mamlaka kulingana na wakili wao.

Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi ambalo tangu 2005 limekuwa chini ya utawala wa rais Faure Gnassingbe, limekuwa likilaumiwa na makundi ya kutetea haki kwa msako dhidi ya viongozi wa upinzani na vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa wa shirika la habari la AFP, Ferdinand Ayite na Koukou Kouwonou ambaye pia anajulikana kama Isidore Kouwonou, ambapo Ayite ni mkurugenzi na Kouwonou mhariri wa jarida linalochapishwa kila wiki mbili la Alternative, walishtakiwa Desemba 2021, kwa tuhuma za kuidharau mamlaka pamoja na kueneza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo ilifuatia malalamiko kutoka kwa waziri wa sheria Pius Kokouvi Agbetomey na mwenzake wa biashara Kodjo Adedze juu ya video iliyorushwa na wanahabari hao kwenye mtandao wa YouTube. Kulingana na wakili wao Elom Kpade, mahakama katika mji mkuu wa Lome imewapa hukumu ya kifungo cha miaka 3 jela pamoja na faini ya dola za kimarekani 4,900 kila mmoja.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa kwao ilikuwa imetolewa awali dhidi yao, lakini ameongeza kusema kwamba atashauriana na wateja wake kuhusu uwezekano wa kukata rufaa. Ayite alikamatwa kwa muda pamoja na mwanahabari mwingine Desemba 2021, lakini kwa sasa yeye na Kouwonou wanaishi mafichoni.

XS
SM
MD
LG