Tume ya Ulaya ilisema ilikuwa imetuma maombi rasmi ikitaka taarifa kutoka Meta na TikTok mtawalia ikiwa ni utaratibu wa kwanza uliozinduliwa chini ya sheria mpya ya EU kuhusiana na maudhui ya mtandaoni.
EU ilizindua uchunguzi kama huo wiki iliyopita kwa bilionea Elon Musk kwa mtandao wake wa kijamii wa X ambapo zamani ulikuwa ukijulikana kama Twitter.
Tume hiyo ilisema ombi hilo lililotumwa kwa Meta kuhusiana na “usambazaji na utangazaji wa maudhui yanayokiuka sheria na taarifa potofu” kuhusu mgogoro wa Hamas na Israel.
Katika taarifa nyingine, ilisema ilitaka kujua zaidi kuhusu juhudi za TikTok katika kuzuia usambazaji wa maudhui ya kigaidi na ghasia na matamko ya chuki.
Kitengo cha kiutendaji wa EU uliongeza kuwa ulikuwa unataka taarifa zaidi kutoka Meta kuhusu “hatua za udhibiti katika kulinda heshima ya chaguzi mbalimbali”.
Meta na TikTok wamepewa hadi Oktoba 25 kujibu hoja hiyo, na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha taarifa Novemba 8 kwa vipengele ambavyo si muhimu sana kuhusu mahitaji ya taarifa
Tume hiyo ilisema imetaka maelezo zaidi kuhusu TikTok vipi inatekeleza kanuni za kuwalinda watoto katika mitandao.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.