Ukraine yaeleza Russia imepata mafanikio ya kiasi katika vita

Magari ya kijeshi yaendelea kutumia barabara, katikati ya uvamizi wa Russia huko Ukraine, katika Mkoa wa Donetsk.

Jeshi la Ukraine linasema vikosi vya Russia vimepata mafanikio kiasi katika mji wa mashariki wa Severodonetsk na kuvisukuma vikosi vya Ukraine nje ya mji huo.

Kwa msaada wa mizinga, mashambulizi katika mji huo yalikuwa yanaendelea, msemaji wa vikosi vya jeshi la Ukraine Oleksandr Shtupun alisema Jumatatu.

Msemaji wa vikosi vya Ukraine Oleksandr Shtupun anaeleza:“ Katika mwelekeo wa Severodonetsk, adui kwa msaada wa mizinga, amefanya operesheni za mashambulizi katika mji wa Severedonesky na kufanikiwa kwa kiasi kuvisukuma vikosi vyetu nje ya mji. Mapigano yanaendelea. Wanajeshi wa Russia wamefyatua makombora katika maeneo ya jeshi la ulinzi kwenye makazi ya Lysichank, Severodonetsk, na Toshkivka.

Wiki nne sasa Severodonetsk imekuwa lengo la mashambulizi ya mabomu la Russia huko Ukraine.

Ripoti zinasema takriban asilimia 70 ya mji uko chini ya udhibiti wa Russia na vikosi vya Ukraine vimesukumwa nje ya mji na adui mwishoni mwa wiki.