Nchi hiyo yenya idadi kubwa ya vifaru duniani ni kitovu kikuu cha ujangili, unaosababishwa na mahitaji ya Asia, ambako pembe zinatumika kwa dawa ya asili kwa imani inaleta afwen ya haraka kwa wagonjwa.
Wizara ya mazingira imesema kuwa mbali na jitihada za serikali kukabiliana na biashara hiyo haramu, idadi ya wanyama hao 499 wenye ngozi nene wanaokula majani waliuawa mwaka 2023, hususani katika mbuga zinazosimamiwa na serikali. Idadi hii inawakilisha ongezeko la aslimia 11 kulingana na takwimu za mwaka 2022.
Takwimu inatoa taswira ya kutisha, kulingana na shirika la kuwalinda vifaru, 'Save the Rhino', linalotoa wito wa kupatikana rasilimali za dharura ili kupambana na magengi ya ujangili.
Serikali inasema kwamba idadi kubwa ya vifaru wanao windwa ni kiatika jimbo la mashariki la KwaZulu-Natal ambako kunapatikana hifadhi kongwe ya Hluhluwe–Imfolozi—peke yake imepoteza wanyama 307.