Ugiriki yazikumbusha nchi za Mediterranean janga la hali ya hewa

Kyriakos Mitsotakis

Nchi za Mediterranean lazima ziongoze katika kutafuta ufumbuzi wa mabadiliko ya hali ya hewa, Waziri Mkuu wa Ugiriki amesema.

voaWaziri Mkuu pia ameonya kuwa gharama ya kutofanya lolote haikadiriki, huku inawezekana wanadamu wakawa wanahangaika kuendelea kuishi kufikia karne inayokuja.

Ugiriki, Uturuki, Cyprus na Uhispania zilikuwa zimeathiriwa na mioto ya misitu na kuwa na viwango vya juu vya joto katika majira ya joto mwaka 2021, huku wanasayansi wakionya kuwa eneo hilo limegeuka kuwa ni “uwanja wa mioto ya misituni.” Ujerumani, Uturuki na China ziliathiriwa na uharibifu uliotokana na mafuriko.

“Sitaki kuendelea kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa. Nataka kuzungumzia kuhusu mgogoro wa hali ya hewa, tayari uko hapa,” Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis ameiambia Reuters katika mahojiano."

“Na ili kulitatua hili, tunahitaji sera pana ambazo zinaingiliana na kila nyanja ya uchumi wetu na maisha yetu ya kijamii.”

Jopo la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa joto lenye hatari, vimbunga vikubwa na hali nyingine za hewa hatarishi zitaendelea kuongezeka.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters