Sheria iliyosainiwa na Rais Yoweri Museveni inatoa adhabu ya kifo kwa "ushoga uliokithiri," kosa ambalo ni pamoja na kusambaza UKIMWI kupitia ngono ya mashoga.
Kupitishwa kwa sheria hiyo kulitangazwa siku ya Jumatatu, na kwa haraka imekemewa na serikali za Magharibi na kuhatarisha baadhi ya mabilioni ya dola za misaada ya nje ambayo nchi hiyo inapokea kila mwaka.
Rais wa Marekani Joe Biden alitishia kupunguza misaada na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vingine, huku Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akisema serikali itazingatia vya visa dhidi ya maafisa wa Uganda. Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema sheria hiyo itaathiri uhusiano wa Uganda na washirika wa kimataifa.
Maoni ya awali ya kina kutoka serikali ya Uganda, tangu Museveni atie sheria hiyo, Waziri wa Habari Chris Baryomunsi alipuuza lawama hizo.
"Hatuuoni ushoga kama haki ya kikatiba. Ni upotevu tu wa kijinsia ambao hatuungi mkono kama Waganda na Waafrika,"waziri huyo aliliambia shirika la habari la Reuters.
"Wakati tunathamini msaada tunaoupata kutoka kwa washirika, lazima wakumbushwe kwamba sisi ni nchi huru na hatutungi sheria kwa ajili ya nchi za Magharibi. Tunatunga sheria kwa ajili ya watu wetu hapa Uganda. Kwa hivyo usaliti wa aina hiyo haukubaliki."
Wanaharakati na mawakili nchini Uganda walifungua kesi siku ya Jumatatu kuipinga sheria hiyo. Walisema inahimiza ubaguzi na unyanyapaa na kudai kuwa sheria hiyo imepitishwa bila ya kuushirikisha umma ipasavyo.
Chanzo cha habai hi ni Shirika la habari la Reuters