Rais wa Uganda Yoweri Museveni siku ya Jumatatu alitia saini kuwa sheria mswaada wenye utata wa kupinga mapenzi ya jinsia moja, ofisi yake na bunge la nchi hiyo wamesema na kupitisha adhabu kali sana dhidi ya ushoga.
Museveni ameukubali mswaada wa kupinga ushoga wa mwaka 2023. Sasa unakuwa Sheria ya Kupambana na Ushoga 2023, taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya Twitter ya urais ilisema. Bunge la Uganda kupitia ukurasa wake wa Twitter limesema Museveni ameidhinisha rasimu mpya ya sheria hiyo ambayo ilipitishwa kwa wingi mwezi huu na wabunge ambao walitetea hatua hizo kama kulinda utamaduni na maadili ya taifa.
Rais alikuwa amewataka wabunge kuufanyia marekebisho mswaada huo, ingawa vipengele vingi vyenye msimamo mkali ambavyo vilisababisha ukosoaji katika nchi za Magharibi na onyo la athari za kidiplomasia vimeendelea kuwepo.
Forum