Tume ya uchaguzi ya Nigeria imeanza kutangaza matokeo ya kura za urais kutoka kwene majimbo, katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi.
Mshindi anatarajiwa kutangazwa baada ya siku kadhaa na kuchukua nafasi ya Muhammadu Buhari, ambaye amemaliza muda wake kikatiba.
Obi, wa chama cha Leba, amepata kura 582,454, akifuatiwa na aliyekuwa gavana wa Lagos Bola Tinubu wa chama cha All progressive Congress.
Tinubu amekuwa na ufuasi mkubwa katika jimbo la Lagos kwa miaka mingi.
Kiongozi wa upinzani Atiku Abubakr, wa chama cha Peoples Democratic Party, amepata kura 75,750.
Kampeni ya Obi imekuwa ikiwahimiza wapiga kura kuwakataa washindani wake kutoka vyama ambavyo vimeiongoza Nigeria kwa robo karne, na ambao uongozi wao umejaa ufisadi na ukosefu wa usalama.
Nigeria ni nchi yenye idadi kubwa ya watu Afrika.