Kampuni ya mitandao ya kijamii ya China TikTok siku ya Alhamisi iliahidi kufanya zaidi kukabiliana na upotoshaji wa habari kwenye jukwaa lake kwa kuongeza vidhibiti zaidi vya usalama na kuongeza uthibitishaji wa usahihi wa habari.
Hali hii imechochewa na jukumu la vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali na vita nchini Ukraine, Reuters iliripoti.
Ikiwasilisha ripoti yake ya maendeleo ya kukidhi kanuni za utendaji za Umoja wa nchi za Ulaya kuhusu upotoshaji wa habari miezi sita iliyopita, kampuni hiyo imekiri inahitaji kuongeza juhudi.
Wakati tunajivunia kutoa kiwango hiki cha maelezo ya kina kwa mara ya kwanza, tunatambua kuwa kuna kazi ya kufanywa. Katika miezi ijayo, tunawekeza katika juhudi kadhaa”, Caroline Greer, mkurugenzi wa sera za umma na mahusiano ya kiserikali, alisema kwenye chapisho la blogi.
TikTok itapanua nembo zake za vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali, na kuongeza jitihada dhidi ya upotoshaji wa habari zinazohusiana na Ukraine kwa kupanua programu zake za kuangalia ukweli wa habari kwa nchi zote za Ulaya na kuongeza lugha zinazotumika pamoja usahili wa habari, alisema Caroline Greer.