Akieleza mafanikio na changamoto ya sera yake ya mambo ya nje katika hotuba yake ya hali ya kitaifa kwenye Bunge Jumanne usiku, rais alielezea matumaini na sauti ya kupinga, akilenga matamshi yake kwa chama cha Kikomunisti cha China na kiongozi wa Russia Vladimir Putin.
Siku chache baada ya puto la kijasusi la China kuingia katika anga ya marekani, kulisababisha kuahirishwa kwa safari ya ngazi ya juu ya waziri wa mambo ya nje Antony Blinken, rais Biden alieleza anachokiona hivi sasa katika uhusiano na Beijing.
Rais alisema bado yuko tayari kufanya kazi na China, "ambayo inaweza kuendeleza maslahi ya Marekani na kuinufaisha dunia."
"Lakini tusifanye makosa," alisema. "Kama tulivyoweka wazi wiki iliyopita, ikiwa China itatishia uhuru wetu, tutachukua hatua kulinda nchi yetu, na mefanya hivyo."