Maafisa wa Ukraine wametoa wito kwa washirika wao wa Magharibi kutuma ndege hizo ili kukabiliana vyema na uvamizi wa Russia, lakini hadi sasa wito huo umepokelewa kwa tahadhari.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kama Ufaransa inamipango ya kutuma ndege za kivita nchini Ukraine, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumatatu kwamba hakuna kisichojadiliwa lakini aliweka masharti mengi kabla ya hatua hiyo kuchukuliwa. Hizo ni pamoja na kwamba vifaa hivyo havingegusa ardhi ya Russia, haingesababisha kuongezeka kwa mvutano na haitadhoofisha uwezo wa jeshi la Ufaransa.
Nchini Marekani, Rais Joe Biden alipowasili katika Ikulu siku ya Jumatatu, waandishi wa habari waliuliza ikiwa atatoa ndege za kivita za F-16 kwa Ukraine. Biden alijibu, Hapana.