Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:56

Hali ya taifa la Marekani ni imara, Biden asema


Rais Joe Biden akiwasili bungeni na kumpa mkono Spika Kevin McCarthy kabla ya kutoa hotuba yake kuhusu hali ya taifa, Februari 7, 2023.
Rais Joe Biden akiwasili bungeni na kumpa mkono Spika Kevin McCarthy kabla ya kutoa hotuba yake kuhusu hali ya taifa, Februari 7, 2023.

Rais wa Marekani Joe Biden alitoa kauli ya matumaini na yenye dhamira wakati wa hotuba yake ya pili kuhusu hali ya taifa la Marekani Jumanne usiku, akipongeza mafanikio yake ya kisheria na kisera.

“Kwa sababu nafsi ya taifa hili ina nguvu, kwa sababu uti wa mgongo wa taifa hili ni imara, kwa sababu wanainchi wa taifa hili wana nguvu, hali ya taifa ni imara,” Biden alisema.

Biden alihutubia bunge ambalo Spika wake Mrepublican Kevin McCarthy, ameapa kutumia wingi mdogo wa warepublican katika Baraza hilo la Wawakilishi kupinga vipaumbele vingi vya Biden.

“Kupambana kwa ajili ya kupambana, kuwania madaraka kwa ajili ya madaraka, mizozo kwa ajili ya mizozo, haitufikishi popote,” alisema.

“Huu umekuwa mtazamo wangu wa nchi yetu kila wakati, na najua ni mtazamo wa wengi kati yenu. Kuboresha nafsi ya taifa hili, kujenga upya uti wa mgongo wa Marekani,” Biden alisema.

UCHUMI WA NCHI

Biden alizungumza kwa kirefu na kwa undani juu ya suala ambalo Wamarekani wanasisitiza ni muhimu kwao.

“Tunajenga uchumi ambapo hakuna mtu atakayeachwa nyuma. Ajira zimerudi kwenye viwango vya juu.”

Biden alisema utawala wake ulibuni rekodi ya ajira mpya milioni 12, ajira nyingi zaidi zilizobuniwa katika miaka miwili kuliko rais yeyote ambaye aliwahi kubuni katika miaka minne.

Biden alitaja miongoni mwa mafanikio yake vita dhidi ya janga la Covid.

“Miaka miwili iliyopita, Covid ilifunga biashara zetu, ilifunga shule zetu, na ilitudhuru sana. Leo, Covid haidhibiti tena maisha yetu.”

XS
SM
MD
LG