Rais wa Algeria Abdulmadjid Tebboune ameshinda uchaguzi wa urais nchini Algeria na ushindi wake kuangaziwa zaidi na vyombo vya habari nchini humo.
Tebboune amepata asilimia 95 ya kura katika uchaguzi wa jana Jumapili na hivyo kutokuwepo kwa duru ya pili ya upigaji kura.
Mshindani wake wa karibu, Abdelaali Hassani Cherif amepata asilimia 3, akifuatiwa na 3 Youcef Aouchiche aliyepata asilimia 2.
Asilimia 48 ya wapiga kura walishiriki zoezi hilo.
Magazeti ya Algeria yamepongeza ushindi wa Tabboune, akisema ushindi wake ni dhihirisho la uthabiti kwa taifa na kwamba anaungwa mkono na watu wengi nchini Algeria.
Baadhi ya raia wa Algeria wamesifu ushindi huo wakisema heri Tabboune wanayemjua vyema kuliko wapinzani wake.
Tebboune, mwenye umri wa miaka 78, anaungwa mkono na jeshi la nchi hiyo.