Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:07

Watu 21 wamekamatwa Algeria kwa madai ya kuingiza kwa magendo silaha


Ramani ya Algeria na nchi jirani
Ramani ya Algeria na nchi jirani

Mwanaume aliyetajwa Moussa Zaidi na mkewe awali walikamatwa Agosti 4 huko Bejaia kiasi cha kilomita 220 mashariki mwa Algiers

Watu 21 wamekamatwa nchini Algeria kufuatia madai ya jaribio la kuingiza kwa magendo silaha kwakutumia usafiri wa ferry kutoka Ufaransa, wizara ya ulinzi nchini humo imesema Jumatano.

Watu wawili, mwanaume mmoja aliyetajwa Moussa Zaidi na mkewe, awali walikamatwa Agosti 4 huko Bejaia, kiasi cha kilomita 220 mashariki mwa Algiers, baada ya maafisa kugundua silaha ndani ya gari lao wakati walipowasili kutoka Marseille, wizara hiyo imesema.

Idara za usalama ziliendelea kuwakamata wanachama wengine 19 wa mtandao huo-huo wa kigaidi na kukamata silaha nyingine nyingi zilizogunduliwa katika kasha la siri karibu na Bejaia, ilisema taarifa hiyo. Wizara ya ulinzi nchini humo imesema kundi hilo ni sehemu ya kundi la Movement for the Autonomy of Kabylie (MAK), ambalo Algeria inaliorodhesha kama “taasisi ya kigaidi”.

Kwa jumla silaha 21 zilikamatwa pamoja na risasi 2,000 pamoja na nguo zinazofanana na sare za jeshi, miongoni mwa mambo mengine, shirika la habari la serikali APS liliripoti Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG