Kwenye taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya kitaifa, Algeria imesema kwamba imepokea mwitikio rasmi kutoka Niger kufuatia mwaliko wa rais Abdelmadjid Tebboune. Hata hivyo hakuna majibu yaliotolewa moja kwa moja na utawala wa kijeshi wa Niger.
Algeria imekuwa ikionya dhidi ya mwingilio wa kijeshi katika kutatua mzozo wa Niger ambapo walinzi wa rais walifanya mapinduzi na kuanza utawala wa kijeshi, wakisema kwamba watahitaji miaka mitatu ya kukamilisha mchakato wa mpito.
Mwishoni mwa Agosti, waziri wa kigeni wa Algeria Ahmed Attaf alisema kwamba Algeria mara kadhaa imezungumza na viongozi wa kijeshi wa Niger, na kupendekeza mchakato wa kurejesha taifa hilo kwenye utawala wa kikatiba.
Forum