Pande mbili zinazozozana zilionekana kuelekea kwenye vita vya pande zote kufuatia miezi kadhaa ya mvutano unaozidi kuongezeka.
Roketi hizo zilizorushwa usiku kucha zilisababisha ving'ora kulia, vikionya kuhusu mashambulizi ya kupitia angani, na kupelekea maelfu ya watu kukimbilia kwenye makazi.
Jeshi la Israel limesema roketi zimerushwa "kuelekea maeneo ya raia." Hali hiyo iliashiria uwezekano wa kuongezeka kwa uhasama baada ya mashambulio ya awali kulenga shabaha za kijeshi.
Israel ilianzisha mamia ya mashambulizi kwa kile ilichosema ni malengo ya wanamgambo. Mtu mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa kusini mwa Lebanon.
Takriban watu wanne walijeruhiwa na mabomu huko Israel. Roketi moja ilipiga karibu na jengo la makazi huko Kiryat Bialik, jamii karibu na Haifa, na kujeruhi watu wasiopungua watatu na kuchoma moto majengo na magari.
Kikosi cha uokoaji cha Israel Magen David Adom kilisema kuwa jumla ya watu wanne walijeruhiwa na mabomu katika shambulio hilo.