Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:31

Mashambulizi kati ya Israel na Hezbollah yaongezeka


Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ametoa wito kwa wanachama wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta namna ya kupunguza uhasama kati ya Israel na Lebanon.

Dujarric amesema hayo wakati mgogoro unaongezeka kwenye mpaka wa Lebanon na Israel.

Amesema kwamba katibu mkuu na maafisa wa ngazi ya juu wamekuwa wakifuatilia kwakaribu sana hali kusini mwa Lebanon na kaskazini mwa Israel.

Mratibu maalum kwa ajili ya Lebanon Jeanine Hennis Plasschaert amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na wahusika akiwasihi kupunguza uhasama na kuruhusu utulivu pamoja na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia ili kumaliza machafuko haraka iwezekanavyo.

Uhasama kwenye mpaka wa Lebanon na Israel umekuwa ukiongezeka tangu Oktoba 8 2023, wanamgambo wa Hezbollah waliporusha makombora kuelekea Israel kuonyesha mshikamano na wanamgambo wa Hamas.

Israel ilijibu roketi za Hezbollah kwa msururu wa makombora kuelekea kusini mwa Lebanon.

Watu 37 wakiwemo watoto wameuawa. Maelfu wamejeruhiwa na baadhi wapo katika hali mahututi baada ya vifaa vya mawasiliano vilivyokuwa mfukoni au mikononi kulipuka

Stephane Dujarric – msemaji wa Katibu Mkuu wa UN anaeleza: "Tunaendelea kuomba pande husika kutekeleza azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa namba 1701 na kurejesha utulivu. Ni muhimu kwamba nchi wanachama zinachangia katika kumaliza uhasama huo.

Forum

XS
SM
MD
LG