Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 22, 2024 Local time: 22:25

Wanajeshi wa Israel wameshika doria mpakani na Lebanon


Shambulizi la Israel katika kijiji cha Kfar Kila, kilichoko kusini mwa Lebanon, karibu na mpaka na Israel Sept. 20, 2024.
Shambulizi la Israel katika kijiji cha Kfar Kila, kilichoko kusini mwa Lebanon, karibu na mpaka na Israel Sept. 20, 2024.

Wanajeshi wa Israel wameshika doria katika eneo linaloshikiliwa na Israel la Golan Heights wakati hali ya wasiwasi inayoendelea kuongezeka mpakani mwa Israel na Lebanon.

Hayo yanajiri baada ya kiongozi wa Hezbollah kuapa kuendelea na mashambulizi ya kila siku dhidi ya Israel, licha ya matukio ya wiki hii ya vifaa vingi vya mawasiliano vya Hezbollah kulipuka, na kusema kwamba raia wa Israel waliokoseshwa makazi karibu na mpaka na Lebanon hawataruhusiwa kurudi hadi vita vya Gaza vitakapomalizika.

Hezbollah na Israel wamekuwa wakishambuliana mpakani wakati Hassan Nasrallah alikuwa akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kulipuka vifaa vya mawasiliano vya Hezbollah, tukio ambalo amelitaja kuwa pigo kubwa na kuahidi kulipiza kisasi.

Israel imelaumiwa kwa mashambulizi ya siku mbili dhidi ya vifaa vya mawasiliano vya mkononi vya Hezbollah, katika matukio ambayo yameongeza hofu kwamba mapambano ya kila siku ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 11 kati ya Hezbollah na Israel huenda yakaongezeka na kuwa vita kamili.

Katika wiki za hivi karibuni, viongozi wa Israel wamekuwa wakionya kwamba kuna uwezekano wa kufanya operesheni ya kijeshi dhidi ya Hezbollah, ikisema kwamba inalenga kumaliza mashambulizi ya kundi hilo ili kuruhusu maelfu ya waisrael wanaoishi mpakani kurudi nyumbani.

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema kwamba kundi la Hezbollah litalipia gharama kubwa wakati Israel inalenga kuhakikisha kwamba raia wake wanaoishi karibu na Lebanon wapo salama.

Forum

XS
SM
MD
LG