Somaliland yakataa pendekezo la Museveni, yasema haina mpango wa kufanya mazungumzo kujadili umoja

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Somaliland imesema haina mpango wa kufanya mazungumzo ya kujadili umoja, baada ya rais Yoweri Museveni kutoa pendekezo la kuwa mpatanishi kati ya nchi hiyo inayojitangazia jamhuri na serikali ya shirikisho ya Somalia.

Rais Museveni jumamosi alisema kwamba amekubali kuchukua jukumu la mpatanishi wa amani baina ya makundi mawili baada ya Mkutano na mjumbe wa serikali ya Somaliland mjini Entebe nchini Uganda.

Amesema uganda haiungi mkono kujitenga kwa jamhuri hiyo kwa sababu kimkakati ni makosa.

Lakini katika taarifa, waziri wa mambo ya nje wa Somaliland alisema kwamba mazungumzo yoyote na serikali mjini Mogadishu hayatajadili kuungana lakini badala yake itakuwa ni jinsi gani nchi hizo mbili zilizoungana hapo awali zinaweza kusonga mbele kila moja peke yake.

Kwa hiyo jamhuri ya Somaliland kwa mara nyingine tena imethibitisha kwa umoja wa afrika na jumuiya yote ya kimataifa kwamba haina mpango wowote wa kufanya majadiliano ya umoja na somalia. Imeongeza kusema taarifa hiyo.