Shirika la ufadhili la Uingereza, Save The Children, linasema uvamizi wa nzige, hali mbaya ya hewa na uhaba wa mvua vitasababisha mamilioni ya wananchi wa Somalia kutokuwa na chakula cha kutosha mwaka 2021.
Shirika hilo linasema uzalishaji wa chakula na mboga unatarajiwa kushuka kwa asilimia 80 mnamo msimu huu.
Mapato kutoka biashara kuu ya ufugaji nchini Somalia inatarajiwa ksuhuka kwa asilimia 55.
Save the children linasema kina mama wanahangaika kutafuta angalau chakula cha mara moja kwa siku kwa watoo watoto wao.
Makadirio yanatabiri kuwa mwaka huu familia maskini kusini mwa Somalia wataweza kuvuna asili mia 15 tu ya mazao yao ambapo wakati wa misimu mizuri walifanikiwa kupata hadi nusu ya chakula kutokanan na mazao yao.