Shambulizi katika hospitali ya Al Shifa halikuwalenga raia - jeshi la Israel

Wapalestina wakiwabeba majeruhi katika hospitali ya Al Shifa Gaza City Novemba 9, 2023. Picha na REUTERS/Doaa Rouqa

Wanajeshi wa Israel waliingia katika hospitali Al Shifa, ambayo ni kubwa kuliko zote katika eneo la Gaza siku ya Jumatano, na kufanya msako katika majengo ya hospitali hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Israel kusema wapiganaji wa Hamas walikuwa katika njia zilizojengwa chini ya hospitali, tuhuma ambazo kundi hilo la Wapalestina linakanusha.

Haya hapa ni majibu kuhusiana na mapigano yalitokea Al Shifa na hospitali nyingine zilizipo Gaza:

ISRAEL

Kulingana na habari za kijasusi, "vikosi vya IDF vinafanya operesheni kwa usahihi na inayolengwa dhidi ya Hamas" katika maeneo ya hospitali lengo halikuwa kuwadhuru raia, Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema katika taarifa.

Wanajeshi wa Israeli waligundua silaha na "miundombinu ya kgaidi" katika eneo moja maalum ndani ya hospitali ya Al Shifa, afsia mwandamizi wa IDF alisema.

Hakuna mapigano ndani ya jengo la hospitali baada ya askari kufika wakati wa usiku, na wafanyakazi wa hospitali na wagonjwa walikuwa katika eneo jingine tofauti, alisema.

Madaktari wakiangalia uharibifu katika wodi za hospitali ya Al Shifa kufuatia shambulio la Israel, Novemba 15, 2023. Picha na Wizara ya Afya ya Gaza/Kitini /REUTERS

HAMAS

"White House na Pentagon wanachukua uwongo wa taarifa ya (Israeli) , inayodai kwamba upinzani unatumia majengo ya hopitali ya Al Shifa kwa madhumuni ya kijeshi, alikuwa taa ya kijani kwa uvamizi (Israel) kufanya mauaji zaidi dhidi raia," Hamas ilisema.

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

"Ripoti za uvamizi wa kijeshi katika hospitali ya Al Shifa unatia wasiwasi sana," Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X. "Tumepoteza mawasiliano tena na wafanyikazi wa afya walioko hospitalini. Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao na wa wagonjwa wao'

MKUU WA MISAADA WA UMOJA WA MATAIFA

"Ulinzi wa watoto wachanga, wagonjwa, wafanyakazi wa hospitali na raia wote lazima upewe kipaumbele kuliko masuala mengine yote," mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths aliandika kwenye mtandao wa X, akiongeza "alishtushwa" na ripoti za uvamizi huo. "Hospitali sio uwanja wa vita."

wanajeshi wa Israel wakati wa operesheni ya kijeshi jirani na hospitali ya Al-Shifa Picha na Vikosi vya Ulinzi vya Israeli / AFP

DAKTARI KATIKA HOSPITALI YA AL SHIFA

"mabomu. Risasi ziliizunguka nje na ndani ya hospitali. Inatisha sana unaweza kuhisi kuwa risasi ziko karibu sana na hospitali. Na baadaye tukagundua kuwa mizinga ilikuwa ikisonga karibu na hospitali," Daktari Ahmed El Mokhallati aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.

"Walikuwa wameegesha tu mbele ya idara ya matibabu ya dharura. Kila aina ya silaha zilitumika kuizunguka hospitali," na wafanyakazi waliepuka kuwa karibu na madirisha.

Alisema alijisikia ahueni wakati askari hatimaye walipoingia kwenye jengo hilo, licha ya wasiwasi mkubwa wa miongoni mwa wafanyakazi kuwa na hofu ya kulipuliwa na mabomu kutoka nje.

MAREKANI

"Hatuungi mkono mashambulizi ya anga katika hospitali na sisi hatutaki kuona milipuko ya moto hospitalini ambako kuna watu wasio na hatia, wasiojiweza, wagonjwa wanaojaribu kupata matibabu wanayostahili wananaswa katika mapigano," Msemaji wa Ikulu ya Marekani wa Baraza la Usalama la Taifa alisema."Hospitali na wagonjwa lazima walindwe."

Chanzo cha taarifa hii ni Shirika la habari la Reuters