Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:12

Jeshi la Israel lavamia hospitali ya Al Shifa, huko Gaza


mMama Mpalestina akiwasilishwa hospitali Gaza baada ya jengo lake kubomolewa alfajiri ya Jumatano Nov, 15, 2023.
mMama Mpalestina akiwasilishwa hospitali Gaza baada ya jengo lake kubomolewa alfajiri ya Jumatano Nov, 15, 2023.

Jeshi la Israel linasema limeshambulia hospitali kuu ya huko Gaza katika operesheni kuilenga kambi kuu ya wanamgambo wa Hamas, linadai iko chini ya jengo la hospitali yenye maelfu ya raia wagonjwa na waliopewa hifadhi huko.

Licha ya onyo kutolewa na Marekani na mataifa mengine kwamba hospitali hiyo ya Al Shifaa ni lazima ilindwe, Jeshi la Ulinzi la Israel IDF, limesema kwamba wakati wa alfajiri wanajeshi walingia kwenye uwa mkubwa wa hospitali hiyo.

Katika taarifa yake jeshi linasema kulingana na habari za kijasusi na mahitaji ya kijeshi, wanajeshi wa IDF wanafanya operesheni maalum ya kulenga maeneo maalum ya Hamas katika hospitali ya Al Shifa.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba kuna karibu wagonjwa 2 300, pamoja na wafanyakazi na watu waliokoseshwa makazi ndani ya hospitali hiyo, ambao wamekwama kwa siku kadhaa kutokana na mapigano makali na mashambulizi ya mabomu ya anga.

Mashahidi wameeleza hali ndani ya hospitali ni ya kutisha, ambako matibabu yanafanyika bila bila ya kutumia ganzi. Wanasema hakuna chakula wala maji, huku hewa mahala hapo ni harufu mbaya ya miili inayooza.

Kabla ya shambulio hilo Rais Joe Biden aliihimiza Israel kuchukua tahadhari kubwa kuhusiana na hospitali, akisema ni lazima hospitali kulindwa.

Forum

XS
SM
MD
LG