Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:32

Widodo amtaka Biden kuchukua hatua zaidi za kusitisha vita Gaza

Rais Joe Biden akimkaribisha Rais wa Indonesia Joko Widodo katika ofisi yake ya Oval Office ndani ya White House, Nov. 13, 2023.
Rais Joe Biden akimkaribisha Rais wa Indonesia Joko Widodo katika ofisi yake ya Oval Office ndani ya White House, Nov. 13, 2023.

Rais Joko Widodo, wa Indonesia, taifa lenye idadi kubwa ya waislamu duniani, ametoa wito kwa Rais Joe Biden, wa Marekani kuchukua hatua zaidi kusitisha mateso yanayowapata wananchi wa Palestina, alipokutana na mgeni wake kwenye White House siku ya Jumatatu.

Widodo yuko Washington kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kufikia kiwango cha Mshirika kamili wa Usalama na Ulinzi, viwango vya juu kabisa vya kidiplomasia vya Marekani.

Akizungumza kabla ya mkutano wake na Biden katika Ikulu, Widodo alisema nchi yake ina matumaini ushirikiano huo mpya utachangia katika amani ya kikanda na kimataifa.

Rais Joe Biden wa Marekani akizungumza na mgeni wake Rais wa Indonesia Joko Widodo,katika ofisi yake kwenye White House Novemba 13, 2023.
Rais Joe Biden wa Marekani akizungumza na mgeni wake Rais wa Indonesia Joko Widodo,katika ofisi yake kwenye White House Novemba 13, 2023.

Hivyo aliendelea kusema kwamba “Indonesia inatoa wito kwa Marekani kufanya juhudi zaidi kusitisha mateso huko Gaza,” akiongeza kwamba “usitishaji mapigano ni lazima ufanyike kwa ajili ya ubinadamu.”

Biden alitaja orodha ya mambo yenye maslahi ya pamoja ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa usalama katika usafiri wa baharini, kujenga mfumo thabiti wa uchukuzi wa bidhaa, na mpito kuelekea nishati mbadala ili kupambana na mzozo wa hali ya hewa.

Hakutaja suala la vita vya Gaza. Lakini baadae aliitaka Israel kuchukua tahadhari zaidi katika kuwalinda raia.

Moto mkubwa na mosi unaotanda hewani baada ya shambulio la bomu kwenye Ukanda wa Gaza ukionekana kutoka Israel Kusini .
Moto mkubwa na mosi unaotanda hewani baada ya shambulio la bomu kwenye Ukanda wa Gaza ukionekana kutoka Israel Kusini .

Viongozi hao wawili wanatofautiana kabisa juu ya ugomvi huo, pale Biden akiunga mkono Israel bila ya kutetereka na Widodo akidai kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza.

Widodo anaunga mkono pia tume ya Umoja wa Mataifa ambayo imekua ikikusanya ushahdii wa uhalifu wa vita unaotendwa na pande zote mbili tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7.

Forum

XS
SM
MD
LG