Nchi hiyo pia imeweka masharti ya kujiweka KARANTINI kwa siku saba kwa wasafiri wote wanaowasili Kigali ambao hivi karibuni walikuwa katika nchi zilizoathiriwa na corona.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Rwanda inafanya haya kwa ajili ya kudhibiti maambukizo ya kirusi kipya kilichogunduliwa Afrika Kusini na nchi jirani wiki iliyopita na kutangazwa Novemba 25.
Kirusi cha Omicron tayari kimethibitishwa katika nchi 13. Maamuzi hayo yalifanyika baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri Jumapili kilichokuwa kinajadili jinsi ya kupambana na kirusi hicho.
Kikao hicho kiliongozwa na Rais Paul Kagame. Rwanda inaungana na Umoja wa Ulaya, Marekani, Israeli, nchi za Jumuiya ya Kiarabu, Uingereza miongoni mwa nchi nyingine ambazo zimesimamisha safari zake kwenda kusini mwa AFrika.