Kesi dhidi ya Griner, mshindi wa medali ya dhahabu mara mbili ya Olimpiki na nyota wa Chama cha Kikapu cha Kitaifa cha Wanawake (WNBA), ilimtumbukiza kwenye mtafaruku wa kisiasa, baada ya Russia kutuma wanajeshi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov alisema Rais Vladimir Putin, na mwenzake wa Marekani Joe Biden walikuwa wamekubaliana hapo awali, kuhusu njia ya kidiplomasia, ambayo inapaswa kutumika kujadili uwezekano wa kubadilishana wafungwa.
"Tuko tayari kujadili mada hii, lakini ndani ya mfumo na njia ambayo ilikubaliwa na marais Putin na Biden," Lavrov alisema wakati wa ziara yake nchini Kambodia.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema Washington iko tayari kushirikiana na Moscow kupitia njia za kidiplomasia zilizowekwa.
Alisema hukumu ya Griner ilikuwa ni mwenelezo wa ukiukaji wa haki zake, baada ya kuzuiliwa kimakosa, na Russia na kuzidisha dhuluma ambayo alikuwa ametendewa.