Kwenye ziara yake ya Mashariki ya Kati Sunak alielezea kuguswa na vifo vya raia kufuatia mashambulizi kati ya Israel na Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa mjini Cairo.
Akizungumza na marais wa Misri na Palestina kwa nyakati tofauti, Sunak alitoa pole kwa rais Mahmoud Abbas ambapo kwa sasa yupo Misri akitazamiwa kuwa mmoja wa watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa amani uliopangwa kufanyika Jumamosi kufuatia kadhia inayoendelea katika ardhi ya Palestina.
Akizungumza na mwenyeji wake Rais Abdel Fattah El-Sisi, Sunak alipongeza "juhudi chanya za Misri pia katika mzozo unaoendelea."
Aidha alihimiza kuendeleza mawasiliano zaidi ndani ya kipindi hiki cha mzozo.
Waziri Mkuu Sunak aliweka wazi kuwa Uingereza inaamini umuhimu wa kutuma misaada kwa watu wa Palestina na kuifikisha kupitia Misri.
Imetayarishhwa na Shafii Mbinda, Sauti ya Amerika, Cairo, Misri.