Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:03

Raia 39 wauawa nchini Sudan wakati mkuu wa jeshi la nchi hiyo akifanya ziara Misri

Picha iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook wa jeshi la Sudan inaonyesha mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akimsalimia Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, baada ya kuwasili katika mji wa pwani wa kaskazini mwa Misri wa El Almein, Agosti 29, 2023

Mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Burhan Jumanne alisafiri kwenda Misri kwa mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, huku kukitokea mauaji ya raia kadhaa katika mkoa wenye mzozo wa Darfur.

Wakati Abdel Fattah al-Burhan akiondoka nchini kuelekea Misri, madaktari na mashahidi wamesema raia 39 waliuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, katika shambulio la makombora huko Nyala, mji wa pili katika jimbo la Darfur Kusini ambako mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yamepamba moto.

Ni ziara ya kwanza ya Burhan nje ya Sudan tangu kuzuka kwa mzozo kati yake na kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces (RSF) katikati mwa mwezi Aprili.

Taarifa ya jeshi imesema mazungumzo yao yatajumuisha matukio ya hivi karibuni nchini Sudan na uhusiano kati ya Sudan na Misri.

Mwezi Julai, El-Sissi aliongoza mkutano wa nchi jirani na Sudan ambao ulipendekeza mpango wa kusitisha mapigano.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano hayakudumu.

Forum

XS
SM
MD
LG