Rais Xi akutana na viongozi wa Afrika

Rais Xi Jinping

Rais Xi Jingping wa China amekutana na marais wa Msumbiji, Ethopia, Chile na Mkuu wa Shirika la Fedha duniani, IMF, mjiini Bejing Jumatano kabla ya kuanza mkutano wa kilele cha mradi mkubwa wa miundombinu unaofahamika kama Belt and Road Alhamisi.

Rais Xi aliwakaribisha marais Filipe Nyusi, wa Msumbiji,na Sebastian Pinera wa Chile kwa mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya nchi zao, baada ya kuwapokea kwa heshima za kitaifa.

Baadae kiongozi huyo wa China alikutana na Waziri Mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bi Christian Lagarde kwa mazungumzo mbali mbali.

Karibu viongozi 37 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku mbili kuanzia Alhamisi kujadili mradi mkuu wa Rais Xi wakujenga barabara, reli na bandari kuunganisha nchi yake na nchi za Afrika, Ulaya na Asia, katika lengo la kuimarisha ushirikiano.

Marekani inapeleka ujumbe wa maafisa wa ngazi ya chini kutokana na mvutano ulioko kati ya nchi hizi mbili kuhusiana na mradi huo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.