Uchunguzi wa mara kwa mara wa kimatibabu mapema mwezi huu, ulifichua kwamba Geingob mwenye umri wa miaka 82 alikuwa anaugua saratani, ofisi yake ilisema wiki iliyopita, bila kutoa maelezo kuhusu hali yake.
Rais amekubali ombi la wanasayansi na wataalamu wa matibabu mjini Los Angeles, California, kufanyiwa matibabu mapya ili kukabiliana na seli za saratani, ilisema taarifa ya rais Jumatano, na kuongeza kwamba kwamba atakuwa Marekani kwa wiki moja kabla ya kurejea Namibia kwendelea na matibabu.
Makamu wa rais Nangolo Mumba, atakaimu kama rais wakati Geingob akiwa nje ya nchi.
Wasiwasi kuhusu hali ya afaya ya kiongozi huyo umekuwa ukiongezeka, huku ripoti zikieleza kwamba alikiri mwaka jana, kuwa afya yake ilikuwa imedhoofika. Geingob anatarajiwa kustaafu baadaye mwaka huu, baada ya kuhudumu kwa mihumla miwili kama rais.