Rais wa China atoa mapendekezo ya kuumaliza mzozo wa Ukraine

Rais wa China Xi Jinping (kulia) alipomkaribisha kansela wa Ujerumani Olaf Scholz huko Beijing Novemba 4, 2022. Picha na Kay Nietfeld / POOL / AFP.

Rais wa China Xi Jinping Jumanne ametoa mapendekezo manne ya kujaribu kumaliza mzozo wa Ukraine kuanzia namna ya kudhibiti vita visiene hadi kurejesha Amani.

Xi alikutana na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz huko Beijing, na viongozi hao wawili wamekuwa wakijadili kwa kina na kubadilishana mawazo juu ya maswala ya uhusiano kati ya nchi zao, ikiwa ni pamoja na biashara na mizozo ya Ukraine na Gaza.

Scholz alitegemea kwamba Berlin na Beijing zinaweza kusaidia kufikia amani Ukraine.

Xi amesisitiza kwamba katika hali iliyopo, ili kuzuiya vita kati ya Russia na Ukraine kushindwa kudhibitiwa pande zote hazina budi kufanyakazi kwa pamoja ili kurejesha amani haraka iwezekanavyo.

“kwa sasa , dunia inaishi kupitia mabadiliko ya haraka ambayo hayajawahi kushuhudiiwa katika karne moja na binadamu wanakabiliwa na hatari na changamoto zinazoongezeka. Ili kutatua matatizo haya, ushirikiano kati ya mataifa makubwa ni muhimu.” Rais huyo wa China amesema.