Shirika la taifa la utangazaji nchini humo limeripoti kuwa Rais huyo, maarufu kama Farmajo, "alikuwa amesaini mswaada maalum, wa kutoa mwongozo wa uchaguzi nchini humo, baada ya kupitishwa kwa kauli moja na bunge."
Baraza la wawakilishi la Somalia Jumatatu lilipiga kura ya kuongeza muda wa rais baada ya miezi kadhaa ya makubaliano juu ya kufanyika kwa uchaguzi katika taifa hilo.
Hata hivyo, spika wa Seneti alishutumu hatua hiyo kuwa ni kinyume na katiba, na azimio hilo halikuwasilishwa mbele ya baraza kuu, ambalo kwa kawaida linahitajika, kabla ya kutiwa saini kuwa sheria.
Farmajo na viongozi wa serikali tano za majimbo ya Somalia, walikuwa wamefikia makubaliano mwezi Septemba mwaka jana, kuhusu jinsi ya kufanyika kwa uchaguzi wa moja kwa moja wa bunge na urais mwishoni mwa 2020 na mapema 2021.
Lakini makubaliano hayo yalisambaratika wakati mabishano yalipozuka, na duru nyingi za mazungumzo zimeshindwa kusuluhisha mgogoro huo.