Rais Biden binafsi amehusika katika makubaliano ya kuachiwa kwa mateka Gaza - White house

Rais Joe Biden akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje huko Whte house. Picha na ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP.

Rais Joe Biden “binafsi anahusika" katika makubaliano ya kuhakikisha mateka 50 wanaoshikiliwa huko Gaza na Hamas wanaachiliwa, John Kirby, mratibu wa Baraza la Usalama wa Taifa kwa mawasiliano ya kimkakati, alisema katika mahojiano na VOA siku ya Jumatano.

Kuachiliwa huko kwa sasa kumeahirishwa hadi angalau siku Ijumaa, kutaambatana na kuachiliwa kwa wafungwa 150 wa Kipalestina walioko nchini Israeli, sitisho la muda la mapigano kwa siku nzima na ufikishaji wa misaada zaidi ya kibinadamu huko Gaza.

Kirby, ambaye alizungumza na Paris Huang, mwandishi wa VOA Mandarin anayeripoti White House, pia alipuuza juhudi za hivi karibuni za kidiplomasia za China za kumaliza mzozo wa Israel na Hamas.

Wachambuzi wameelezea jaribio hilo kuwa ni dhamira ya Beijing kujiweka kama anayesimamia anayeaminika katika Mashariki ya Kati kuliko Marekani.

Yafuatayo ni mahojiano yamehaririwa kwa usahihi na ufupi.

VOA: Je, Rais Biden alikuwa na jukumu gani katika makubaliano kati ya Israel na Hamas kuhusu mateka?

MRATIBU WA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA KWA MAWASILIANO YA KIMIKAKATI JOHN KIRBY: Rais alihusika kibinafsi katika ngazi ya kiongozi ili kuona kama tunaweza kufanikisha mpango huu. Kwa hakika, alikuwa akizungumza na amiri wa Qatar wiki iliyopita tu wakati tulipokuwa San Francisco kwa ajili ya kongamano la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki. Amekuwa akiarifiwa, wakati mwingine mara kadhaa kwa siku, kuhusu jinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea na mazungumzo. Na bila shaka, aliagiza timu nzima ya usalama wa taifa kufanya kazi kwa bidii kuleta matokeo haya, kuanzia kwa mkurugenzi wa CIA hadi waziri wa mambo ya nje na mshauri wa usalama wa kitaifa. … Na bila shaka, mjumbe maalum katika eneo hilo David Satterfield alikuwa muhimu, kama alivyokuwa mratibu wetu wa Mashariki ya Kati Brett McGurk. Kwa kweli ilikuwa juhudi za timu.

VOA: Wajumbe wa nchi za Kiarabu na Kiislamu walikuwa na mkutano kuhusu Gaza mjini Beijing Jumatatu hii. Je, unaamini mkutano huo unaweza kuwa wa kujenga, na je, Rais Xi aliahidi kusaidia katika suala hili alipokutana na Rais Biden wiki iliyopita?

KIRBY: Nitamruhusu Rais Xi azungumze mwenyewe juu ya kile atakachofanya au hatakifanya. Rais alizungumzia kile kinachoendelea Mashariki ya Kati na Rais Xi na kwa hakika tunamsihi Rais Xi atumie ushawishi wake huko Tehran ili kuhakikisha kwamba tunawasiliana na kiongozi mkuu jinsi tunavyolipa uzito suala hili linaloendelea na kwamba hatutaki kuona vinaongezeka au kusambaa.Na bila shaka, Tehran inaweza kuwa na jukumu katika hilo au la. Na hivyo huo ulikuwa ujumbe thahiri kwa Rais Xi. Lakini China pia ina maslahi katika eneo hilo. Matamanio yetu makubwa ingekuwa waokutumia ushawishi wao katika eneo kwa manufaa zaidi.