Katika taarifa, kamandi hiyo imesema kuwa ndege za kivita za Marekani zilianzisha "mashambulizi ya uhakika dhidi ya vituo viwili nchini Iraq" siku ya Jumatano, nyakati za asubuhi kwa saa za huko katika eneo hilo, ambayo "yalikuwa ni majibu ya moja kwa moja ya mashambulizi dhidi ya Marekani na majeshi ya muungano yaliyofanywa na Iran na makundi yanayoungwa mkono na Iran.”
Mashambulizi ya Marekani yalilenga kituo cha operesheni na kituo cha udhibiti kinachotumiwa na kundi la wanamgambo Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran karibu na Al Anbar na Jurf al-Saqr, afisa wa ulinzi aliiambia VOA.
Siku ya Jumatatu, vikosi vya Marekani vilishambulia na kuwaua washirika wanaoungwa mkono na Iran ambao awali walirusha kombora la masafa marefu dhidi ya kambi ya jeshi la Anga la al-Asad nchini Iraq.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kombora la masafa marefu kurushwa dhidi ya vikosi vya Marekani huko Mashariki ya Kati tangu kuanza mashambulizi ya Oktoba 17, na mara ya kwanza kwa majeshi ya Marekani kulipiza kisasi kwa kuipiga Iraq.
Mashambulizi ya Jumatatu yanayoungwa mkono na Iran yanaashiria kuongezeka kwa mashambulizi yaliyofanywa mwezi uliopita, kwani makombora ya masafa marefu yanaweza kuwa na nguvu zaidi na kufanya uharibifu zaidi kuliko roketi na ndege zisizokuwa na rubani zilizotumiwa katika matukio ya awali.
Forum