Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:47

Qatar yatangaza sitisho la muda la mapigano Gaza


Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi alipokutana na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani huko Cairo, Misri, Novemba 10, 2023. Picha REUTERS
Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi alipokutana na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani huko Cairo, Misri, Novemba 10, 2023. Picha REUTERS

Qatar inatangaza mafanikio ya juhudi zake za pamoja za upatanishi uliofanywa na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Marekani kati ya Israel na kundi Hamas, na kupelekea kwa makubaliano ya kusitisha vita kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Qatar kupitia mtandao wa X, imesema kuwa, "Taifa la Qatar linatangaza sitisho la mapigano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu limekubaliwa huko Gaza"

Muda wa kuanza sitisho hilo utatangazwa ndaniya muda wa saa 24 zijazo na kudumu kwa siku nne, muda huo unaweza kuongezeka.

Wakati huo huo, mfalme Abdullah wa Jordan ameelekea Cairo Jumatano kwa mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi kuhusu jinsi ya kumaliza "uchokozi wa Israel dhidi ya Wapalestina," taarifa ya ufalme ilisema.

Mazungumzo hayo yataangazia jinsi ya kuyafanya makubaliano hayo ya siku nne kati ya Israel na Hamas kuwa sitisho la kudumu ambalo litamaliza mashambulizi ya Israel huko Gaza na kuepusha janga la kibinadamu, afisa mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mfalme Abdullah wa Jordan na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wakiwa Amman Jordan, Januari 13, 2019. Picha na REUTERS/Muhammad Hamed
Mfalme Abdullah wa Jordan na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wakiwa Amman Jordan, Januari 13, 2019. Picha na REUTERS/Muhammad Hamed

Sauti ya Amerika inaripoti kuwa, baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Ukanda wa Gaza kufuatia shambulizi la wanamgambo la mwezi uliopita dhidi ya Israel wanaweza kuachiliwa mapema Alhamisi.

Qatar ilisema Hamas itawaachia wanawake na watoto 50, wakati Israel pia itawaachia "wanawake na watoto wa Kipalestina wanaozuiliwa katika magereza ya Israel."

Makubaliano hayo yaliyotangazwa mapema Jumatano yalikuja baada ya wiki kadhaa za mashauriano yaliyoongozwa na Qatar, Marekani na Misri, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa utawala wa Marekani.

Afisa huyo wa Marekani alisema mateka watakaoachiwa huru na Hamas wanatarajiwa kujumuisha Wamarekani kadhaa.

"Namshukuru Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani wa Qatar na Rais Abdel-Fattah El-Sisi wa Misri kwa uongozi wao thabiti na ushirikiano katika kufikia makubaliano haya," Rais wa Marekani Joe Biden alisema katika taarifa.

"Ninashukuru ahadi ya kweli ambayo Waziri Mkuu Netanyahu na serikali yake waliyotoa katika kuunga mkono sitisho la muda ili kuhakikisha mpango huu unaweza kutekelezwa kikamilifu na kuhakikisha upelekaji wa misaada ya ziada ya kibinadamu ili kupunguza mateso kwa familia zisizo na hatia za Wapalestina huko Gaza."

Forum

XS
SM
MD
LG