Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:41

Mfalme wa Jordan atembelea Misri kuzungumzia mzozo wa Gaza


Mfame wa Jordan Abdullah wa pili. Picha ya maktaba.
Mfame wa Jordan Abdullah wa pili. Picha ya maktaba.

Kiongozi wa Jordan mfalme Abdullah Jumatano amesafiri kuelekea Cairo Misri kwa mazungumzo na rais wa Abdel Fattah al Sisi

.Viongozi hao wanatarajiwa kuzungumzia kuhusiana na namna ya kumaliza mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina, taarifa kutoka makao ya kifalme imesema.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mazungumzo hayo yataangazia sitisho la siku nne la mapigano lililofikiwa kati ya Israel na Hamas, iwapo linaweza kuwa la kudumu, na ambalo litafikisha kikomo mashambulizi ya Israel huko Gaza, ili kuepusha janga la kibinadamu, afisa mmoja ameiambia Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG