Rais Biden asema Marekani iko pamoja na Israeli

Rais Joe Biden akizungumza kuhusu vita kati na kikundi cha wanamgambo Hamas, White House, Washington, Oct. 10, 2023.

Rais Joe Biden akizungumza kuhusu vita kati na kikundi cha wanamgambo Hamas, White House, Washington, Oct. 10, 2023.

Rais Joe Biden alisema Jumanne kuwa “ wako pamoja na  Israeli,” wakati Washington ikijaribu kupunguza mivutano  Mashariki ya Kati baada ya shambulizi la kushangaza la kigaidi lililofanywa na wanamgambo Hamas.

Pia aliahidi Washington itaendeleza msaada kwa Israeli kujibu mashambulizi dhidi ya kile alichokiita “ukatili” ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000, ikiwemo siyo chini ya Wamarekani 14.

“Katika wakati huu, lazima tuwe wazi kabisa: Tunasimama na Israeli,” alisema. “Tutahakikisha wanacho kila wanachohitaji kuweza kuwahudumia raia wao, kujilinda na kujibu shambulizi hili. Hakuna uhalali kwa ugaidi. Na hakuna kisingizio.”

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Biden, akiwa na Makamu Rais Kamala Harris na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, ambao wote walikuwa wanasikiliza kwa makini, alitoa maelezo kuhusu matukio ya wikiendi, ambayo alisema “yalikuwa kitendo cha uovu wa wazi.”

Alisema kuwa ataliomba Bunge kuchukua hatua za haraka” lakini hakufafanu. Kwa sasa, hakuna spika katika Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Warepublikan, inalizuia Bunge kupitisha matumizi mapya.