Pia atasisitiza haja ya utulivu na nguvu ya demokrasia kwa ukuaji wa bara la Afrika.
Rais wa Angola ni mtu maarufu katika bara hilo, alitumia hadhi yake ya uongozi wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta katika eneo ya bara hilo kujenga ushawishi na kufanya kazi katika kusuluhisha mizozo wa kikanda.
Hivi sasa Rais Joao Lourenco anamkaribisha rafiki mpya na mwenye nguvu na kuwa mwenyeji wa Rais Joe Biden katika ziara yake ya kwanza nchini Angola kufanya na rais wa Marekani.
Biden ataitumia ziara hiyo kuangazia ufadhili mkubwa wa Marekani katika mradi wa maendeleo” ujengi wa reli ya Lobito yenye urefu wa kilometa 1,300 ambayo inaunganisha taifa hilo la kiafrika lenye utajiri wa mafuta ndani ya nchi kwenda kwenye bandari iliyopo kusini magharibi. Marekani inasema imekusanya pamoja zaidi yaz dola bilioni 3 fedha binafsi na za umma katika uwekezaji wa Marekani kwenye mradi huu.
White House inasema uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yanapitia “mageuzi ya kweli” wakati wakiwa ni washirika wa karibu sana.
Msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre anasema “kwa pamoja Marekani na Angola zinafanya kazi kushughulikia changamoto mbali mbali zinazojitokeza. Kuanzia kupunguza mwanya wa miundo mbinu Afrika na kukuza fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu katika eneo hilo na kupanua ushirikiano wa kiteknolojia na kisanyansi, na kuboresha amani na usalama, kuimarisha usalama wa chakula.”
Baadhi ya wachambuzi wanasema ahadi ya mwaka 2022 ya Biden kutembelea Afrika imechelewa sana. Biden awali alipanga kwenda Angola mwezi Oktoba, lakini kimbunga Milton kilichotokea nchini kilimfanya aakhirishe safari yake.
Caeron Hudson, wa Kituo cha Mkakati na Masuala ya Kimataifa anasema anadhani kufanyika kwa ziara hiyo mwishoni kabisa mwa utawala wake, bila ya kuwa na mengi ya kufanya, anahisi ziara hiyo haitakuwa na mengi ya kufanya.
Lourenco na Biden hawakubaliani katika kila kitu. Wakati Biden anaiunga mkono Israel kwa ‘dhati kabisa,’ Angola imejiegemeza zaidi katika mtizamo wa Global South.
Rais wa Angola anasema “Israel ina haki ya kujitetea na kulinda maisha ya raia wake, lakini haki kama hiyo pia ni kwa Wapalestina, ambao wamekuwa wakiishi nchini ya ukaliaji mabavu wa kimabavu kwa miongo mingi, hali hiyo haikubaliki.”
Lakini kitu kimoja ambacho wao – na China – wanakubaliana ni haja ya haraka kwa maendeleo ya Afrika. China ina shughuli nyingi katika bara hilo ikiwa na mradi mkubwa sana ambao wameuanzisha wa Belt and Road Initiative.
Xu Jianping wa Tume ya Maendeleo ya Taifa na Mageuzi ya China anasema, katika muda wa miaka 11, makampuni ya China yameshiriki katika ujenzi na ukarabati wa zaidi ya kilometa 10,00 ya nje za reli, karibu kilometa 100,000 ya barabara kuu, na karibu madaraja 1,000, kiasi cha bandari mia kadhaa, na kilometa 66,000 za usambazaji na ujenzi wa njia za umeme, na kilometa 150,000 za mitandao ya mawasiliano ambayo ni uti wa mgongo mwa mataifa mbali mbali ya Afrika.
Wachambuzi wanasema huu si nafasi nzuri kwa bara hilo kuwa ndani.
Ingawa hii ni ziara ya kwanza ya Biden katika eneo hilo lenye utajiri wa dhahabu Afrika, kwa namna fulani , ukurasa wa mwisho. Hii inaonekana ni safari yake ya mwisho ya nje ya nchi, anaiaga dunia kama Rais wa Marekani.